Steven Mukwala amefunga magoli mawili na kufikisha jumla ya magoli 11 kwenye Ligi Kuu bara wakati Simba Sc ikitafuna viporo vyote vinne ikiitandika KMC Fc bao 2-1 katika dimba la KMC Complex.
Simba Sc imesogea mpaka pointi 1 nyuma ya vinara Yanga Sc wakifikisha pointi 69 baada ya mechi 26 huku Wananchi wakiwa na pointi 70 baada ya mechi 26.
FT’ KMC Fc 1-2 Simba Sc
⚽ 08’ Chambo
⚽ 15’ Mukwala
⚽ 47’ Mukwala
MSIMAMO NBCPL
🥇 Yanga SC — mechi 26 — pointi 70
🥈 Simba SC — mechi 26 — pointi 69
🥉 Azam FC — mechi 27 — pointi 54
4️⃣ Singida — mechi 27 — pointi 53
✍️ Nyota wa mchezo wa leo ni Joshua Mutale ‘Budo’