Cyprian Musiba: Yanga Msicheze Dabi Hata Iweje, TFF Wanaendeleza Upendeleo

Cyprian Musiba: Yanga Msicheze Dabi Hata Iweje, TFF Wanaendeleza Upendeleo


Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba, amesema Klabu ya Yanga inapaswa kusimamia msimamo wake wa kutocheza mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba, iliyopangwa kufanyika Juni 15, 2025.

Akizungumza leo Mei 6, 2025, jijini Dodoma, Musiba amesema Serikali haipaswi kukaa kimya huku viongozi wa soka wakiendekeza upendeleo, ushabiki na maslahi binafsi katika uendeshaji wa mchezo huo.

Musiba amesisitiza kuwa anaunga mkono uamuzi wa Yanga kuendelea na msimamo wake wa kususia mechi hiyo, akisema ni hatua ya kulinda heshima ya mpira na uwiano wa haki miongoni mwa vilabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.