Baadhi ya Wananchi na wafanyabiashara jijini Arusha wameipongeza Miaka mitano ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo kuwa ya manufaa kwa kuondoa changamoto zao kwenye Soko kuu, Machinga 68, Samunge, Soko la Krokoni na Kilombero.
Wamesema miundombinu mbalimbali ikiwemo mitaro, Vyoo pamoja na miundombinu ya maji na huduma ya maji safi na salama kuwa changamoto kuu ya Masoko yao, kabla ta Mhe. Gambo kuitatua changamoto hiyo kwa fedha zake binafsi kwenye Masoko yote ya Jiji
"wafanyabiashara hasa wa Soko kuu kwa maana kwamba Mwanzoni hata kudeki maduka ilikuwa shida kwani Idara ya maji iliondoa kabida miundombinu ya maji, sasa hilo likawa tatizo kwa wengi na humu ndani huduma ya vyoo ikawa shida. Leo kila soko limeona matunda ya visima hivi hasa kwa wenye mabucha na wananchi wa pembezoni hapa kwenye mtaa wa bondeni wananufaika na maji haya kwasababu ni ya bure, hayauzwi kwahiyo mnyonge, mnyongeni ila haki yake mpeni." Amesema mmoja wa Wafanyabiashara.
Nao wanawake wanaofanya biashara ya vyakula soko la Samunge, wamemshukuru Mhe. Gambo kwa mitaji, elimu pamoja na majiko ya Gesi waliopatiwa bure na Mbunge huyo, kama sehemu ya kuunga Mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan