Kutokana na Sayansi ya Mpira Nitamtetea Kocha Romain Folz wa Yanga

Kutokana na Sayansi ya Mpira Nitamtetea Kocha Romain Folz wa Yanga


Ameandika Mchambuzi Leo musikula:

 “Simtetei kocha wa Yanga bila sababu za msingi, bali hoja zangu zinatokana na sayansi ya mpira wa miguu.” ⚽ 

1️⃣ Mzigo wa mafanikio ya misimu minne

Yanga imetoka kubeba ubingwa wa Ligi Kuu misimu minne mfululizo. Kila taji limehitaji nguvu kubwa za kimwili na kisaikolojia. Kwenye sayansi ya michezo, wachezaji wanaobeba mzigo mfululizo bila mapumziko ya kutosha huingia kwenye hali ya long-term fatigue – uchovu wa muda mrefu unaohitaji muda kurekebishwa.


2️⃣ Mabadiliko ya wachezaji

Baada ya misimu ya mafanikio, baadhi ya wachezaji wameondoka na wapya kuletwa. Kwenye sayansi ya “team dynamics”, mabadiliko ya nyuso ndani ya timu yanaleta changamoto ya kuunganisha falsafa na mawasiliano. Hii inahitaji muda kabla kikosi kipate muendelezo.


3️⃣ Ulinganisho usioepukika

Mashabiki wanalinganisha kila mechi na Yanga ya misimu iliyopita. Lakini haifai kusahau kwamba “peak performance” huja kwa awamu, na timu inapita kwenye “transition phase” kabla ya kufikia kiwango kipya cha juu.


🔰Hoja ya yangu kuu hapa ni:

Hoja kwamba Yanga haichezi vizuri inaweza ikawa na mashiko kwa jicho la mashabiki, lakini kisayansi, Roman bado yupo kwenye hatua ya kujenga upya mtiririko wa timu baada ya misimu minne yenye mafanikio makubwa na ratiba ngumu. Mchakato huu unahitaji muda, na matokeo kama ushindi wa 3–0 dhidi ya Pamba yanaonyesha bado Yanga ipo kwenye njia sahihi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.