Lissu Atoa Tamko Akiwa Gerezani Baada ya Kuambiwa Wanachama Wanahama Chadema





Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ametoa ujumbe wa moja kwa moja kutoka gerezani Ukonga, ambapo anashikiliwa kwa tuhuma za uhaini.
Katika ujumbe wake uliosambazwa na David Djumbe kupitia mtandao wa X, Mei 11, 2025, Lissu amewasalimu wanachama wa chama chake na kuwataka kuendeleza mapambano ya No Reforms, NoElection, akisisitiza haja ya mageuzi ya uchaguzi na katiba mpya kabla ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Lissu, ambaye alisema atawasili mbele ya safari hivi karibuni, pia aliwatakia heri wale wanaoondoka kwenye chama, akisema, “Wakapambanie wanachoamini.”

Hii inakuja baada ya ripoti za maafisa wa zamani wa CHADEMA (G-55) kujiondoa, na kusababisha uvumi kuhusu mustakabali wa chama hicho.


Kundi la G-55 limeanza kuondika kwenye chama mmoja baada ya mwingine, huku wengi wao wakisema kwamba chama kimepoteza mwelekeo wa kisiasa.

Mtawanyiko hii ilianza baada ya Lissu kuibuka mshindi na kushikilia kitu cha chama kutoka kwa Freeman Mbowe.

Kando na migogoro chamani, Lissu anaendelea kukabiliwa na changamoto za kisheria, huku wafuasi wake wakiahidi kuimarisha harakati za kupigania haki..

Lissu bado ana matumaini ya ushindi.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. AnonymousMay 14, 2025

    Tundu Lissu's call for reforms mirrors SASSA beneficiaries’ struggles when cards are declined—both highlight systemic failures https://sassacheck.net.za/sassa-card-declined/ needing urgent change to ensure fairness, dignity, and reliable public service delivery.

    ReplyDelete