Yule Refa Aliyekataa Bao la Aziz K Kwa Mamelodi Apewa Simba Vs RS Berkane

Yule Refa Aliyekataa  Bao la Aziz K Kwa Mamelodi Apewa Simba Vs RS Berkane


UNAMKUMBUKA yule mwamuzi aliyekataa bao la Stephane Aziz Ki dhidi ya Mamelodi Sundowns lililozua utata mkubwa hadi kwenda kuangaliwa kwenye VAR? Anaitwa Dahane Beida raia wa Mauritania, huyu ndiye ambaye Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemkabidhi jukumu la kuamua mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mkondo wa pili kati ya Simba dhidi ya RS Berkane ya Morocco itakayopigwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa New Amaan, visiwani Zanzibar.

Fainali hiyo imepangwa kuchezwa siku hiyo, baada ya ile ya kwanza itakayofanyika Jumamosi hii huko Berkane, Morocco ikichezeshwa na mwamuzi Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon akisaidiwa na Boris Marlaise Ditsoga (Gabon) na Eric Ayimavo Ayamr Ulrich (Benin), huku refa wa akiba mezani atakuwa Patrice Tanguy Mebiame wa Gabon.

Dahane Beida anakumbukwa kwa tukio la Aprili 5, 2024 lililozua gumzo baada ya shuti la Aziz Ki alilopiga dakika ya 58 dhidi ya Mamelodi Suondowns waliokuwa wenyeji wa mechi ya pili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Afrika Kusini, kwani licha ya mpira kuonekana kudundia ndani, lakini refa huyo alikataa bao baada ya kwenda kujiridhisha kwenye VAR.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.